Oct 8, 2012

RECHO AKIRI HATOWEZA KUACHA KUVAA NGUO FUPI KWANI ZINAMPA UHURU,,,,
RACHEL Haule ‘Recho’ (pichani) anayetamba ndani ya Bongo Movies, amesema hupendelea kuvaa nguo fupi kwa sababu zinampa uhuru katika mitoko yake.
Katika mahojiano maalum na kona hii, Recho alisema nguo fupi si tafsiri kwamba hajiheshimu na anazimikia kwa sababu pia zinamuongezea mvuto na mwenekano wake kuwa wa kisasa zaidi.
“Heshima ya mtu haiwezi kuharibiwa na mavazi, unaweza kuvaa madira na ukawa na tabia za ovyo tu. Mimi najiheshimu lakini siwezi kuacha kuvaa nguo fupi,” alisema Recho.

No comments:

Post a Comment