Oct 3, 2012

SWALA TANO AKUTWA AKIPOMBEKA NDANI YA NIKABU NA BAIBUI,,,


MSANII aliyewahi kutamba na Kundi la Sanaa la Kaole la jijini Dar es Salaam ambaye kwa sasa amejikita kwenye filamu, Mwasiti Mohamed ‘Sishi’ amenaswa katika baa moja iliyopo Sinza–Mori, Dar  mchana kweupe akigida konya au ‘ngumu kumeza’ huku akiwa amevalia  vazi la Kiislamu ‘nikabu’.
Septemba 20, 2012, paparazi wetu alitonywa kuwa, msanii  huyo alitinga kwenye baa hiyo akiwa amevalia nikabu iliyomfunika sehemu kubwa ya juu ya mwili wake na kubakisha uso na alipoketi aliagiza kinywaji hicho na kuwafanya watu kumkodolea macho.
Baadhi ya watu waliokuwa kwenye baa hiyo walipata wakati mgumu kwa kuogopa, wengine wakiamini msanii huyo ni askari ambaye alifika pale kuwakamata watu wanaokunywa muda wa kazi hivyo wengi walikosa amani na kuondoka.
Mwandishi wetu alipomkabili na kumuuliza kulikoni kupiga pombe kali muda ule, alijitetea kuwa eti hakuwa akigida kinywaji hicho, ila alikuwa kwenye baa hiyo akimsubiri mtu kwa ajili ya kufanya makubaliano ya kucheza filamu.
“Mimi sikuwa nakunywa pombe pale, ni maji tu. Nilikuwa namsuburi mtu, aliniambia atakuja, tunataka kuzungumza mambo ya kucheza filamu,” alisema Sishi. 

No comments:

Post a Comment