Oct 17, 2012

YA NGOSWE MWAACHIE NGOSWE DAMN IT,,,,,,


SHEIKH ISSA PONDA AKAMATWA NA POLISI, WAUMINI WAANDAMANA KUSHINIKIZA AACHIWE!!!

Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu, Sheikh Issa Ponda.
KATIBU wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu, Sheikh Issa Ponda amekamatwa na Jeshi la Polisi usiku wa kuamkia leo jijini Dar es Salaam. Sheikh Ponda amekamatwa pamoja na wenzake wapatao 49 wakiwemo wanawake 12, wanaume 37 kwa tuhuma mbalimbali ikiwemo uchochezi dhidi ya Serikali. Kufuatia tukio hilo, baadhi ya waislamu mchana huu wameandamana kwenda kituo cha Polisi Kati kwa ajili ya kushinikiza kuachiwa kwa Sheikh Ponda na waislamu wenzake. Waandamanaji hao walitawanywa na polisi wakati wakijaribu kuingia kituoni hapo.

No comments:

Post a Comment