Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania, Dkt. Alberic Kacou akizungumza machache kuhusiana na umuhimu wa wiki ya Umoja wa Mataifa inayoanza leo ambapo amesema mabadiliko ya hali ya hewa yanayotokea duniani ni ushahidi wa kutosha wa ongezeko la mafuriko na ukame kunakotokana na uharibifu wa mazingira mambo ambayo tunapaswa kuyachukulia kama changamoto kwa kuwa yanatukwaza katika kutimiza malengo ya Maendeleo ya Milenia. Ameongeza kuwa Wiki ya Umoja wa Mataifa kwa mwaka 2012 inaadhimishwa kwa shughuli mbalimbali zinazolenga vijana, wanafunzi, wasomi, vyombo vya habari na jamii kwa ujumla.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bw. John Haule akizungumzia maadhimisho ya miaka 67 ya Umoja wa Mataifa ambapo pamoja na mambo mengine amesema kutakuwa na maonyesho yatakayofanyika katika viwanja vya Karimjee siku ya tarehe 23 na 24 mwezi huu ambapo wananchi wataona mipango na miradi mbalimbali ambayo Umoja wa mataifa umekuwa ukiisaidia Tanzania na pia amesema kutakuwa na mjadala wa wazi katika ukumbi huo siku ya tarehe 23 ambapo wananchi wanakaribishwa kushiriki na kutoa mawazo yao.
No comments:
Post a Comment