Feb 20, 2013

RAIS WA ZANZIBAR DK. SHEIN AONGOZA MAZISHI YA PADRI EVARISTUS MUSHI



 Rais wa Zanbzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt,Ali Mohamed Shein,(katikati) akifuatana na Askofu wa


Kanisa  Katoliki Jimbo la Zanzibar Augustino Shao, wakielekea katika Mazishi ya Padri Evaristus Gabriel  Mushi,aliyezikwa katika viwanja vya kanisa la Kitope,Wilaya ya Kaskazini B Unguja. (Picha na Ramadhan Othman,IKULU)



 Vijana waumini wa Dini ya Kikiristo wakiteremsha jeneza lenye mwili wa marehemu  Padri Evaristus Gabriel  Mushi,katika kaburi alilozikwa  leo katika viwanja vya kanisa la Katoliki la Kitope,Wilaya ya Kaskazini B Unguja,marehemu alifariki kwa kupigwa risasi Jumapili iliyopita na watu wasiojulikanwa.

 Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Tanga Antony Banzi,akiongoza  sala  wakati wa mazishi ya  Marehemu  Padri


Evaristus Gabriel  Mushi,aliyekufa kwa kupigwa risasi Jumapili Iliyopita na kuzikwa leo katika viwanja vya kanisa la Kitope,Wilaya ya kaskazini B Unguja leo.




 Rais wa Zanbzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt,Ali Mohamed Shein,(katikati) akitia udongo  katika


kaburi la Marehemu  Padri Evaristus Gabriel  Mushi,wakati wa mazishi yake yaliyofanyika leo  katika viwanja vya kanisa la Kitope,Wilaya ya Kaskazini B Unguja.



 Askofu wa Kanisa  Katoliki Jimbo la Zanzibar Augustino Shao, akitia udongo katika kaburi la Marehemu Padri



Evaristus Gabriel  Mushi,aliyezikwa leo  katika viwanja vya kanisa Katoliki la Kitope,Wilaya ya Kaskazini B Unguja.



  Waziri  wa  Mambo ya Ndani ya Nchi Emanuel Nchimbi akitia udongo  katika kaburi la Marehemu  Padri Evaristus Gabriel Mushi,wakati wa mazishi yake yaliyofanyika leo  katika viwanja vya kanisa la Kitope,Wilaya ya Kaskazini B Unguja.
ASkofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam Muadham Policup Kadinari Pengo,kwa pamoja na maaskofu wengine wakichomeka Msalaba katika kaburi la marehemu  Padri Evaristus Gabriel Mushi,aliyezikwa leo  katika viwanja vya kanisa Katoliki la Kitope,Wilaya ya Kaskazini B Unguja,ambae alifariki Jumapili Iliyopita kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana.
Waumini wa Dini ya Kikiristo wa Kanisa katoliki na wananchi wakifukia udongo katika kaburi la marehemu  Padri Evaristus Gabriel  Mushi,aliyezikwa leo  katika viwanja vya kanisa Katoliki la Kitope,Wilaya ya Kaskazini B Unguja,ambae alifariki Jumapili Iliyopita kwa kupigwa risasi na watu wasiojukanwa.

Rais wa Zanbzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt,Ali Mohamed Shein,(katikati) akiweka shada la mauwa

katika kaburi la Marehemu  Padri Evaristus Gabriel  Mushi,wakati wa mazishi yake yaliyofanyika leo  katika viwanja vya kanisa la Kitope,Wilaya ya Kaskazini B Unguja. 

No comments:

Post a Comment