Feb 19, 2013

ZIARA YA MAMA JK LINDI YAZIDI KUNOGA, LEO YUPO KATA YA JAMHURI. Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na  Muasisi wa Chama, Mohammed Matipa alipowasili Ofisi ya CCM, Tawi la Tulieni Kata ya Jamhuri Lindi mjini, leo Feb. 19, 2013.
 Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Mama Salma Kikwete akiimba wimbo wa 'Wanawake na Maendeleo', kabla ya kuhutubia mkutano wa hadhara katika kijiji cha  Tulieni, Kata ya Jamhuri Lindi mjini,  leo Feb 19, 2013.
 Wakereketwa wa CCM Mwajabu Abdulrahman (kulia) na Saida Mtopa, wakishangilia wakati Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Mke wa Rais Mama Salma Kikwete alipokuwa akihutyubia mkutano wa hadhara katika kijiji cha Tulieni, Kata ya Jamhiri, Lindi mjini leo, Feb 19, 2013.
 Wanachama wapya wa CCM wakila kiapo baada ya kukabishiwa kadi zao na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Mama Salma Kikwete, katika mkutano wa hadhara uliofanyika leo Feb 19, 2013, kwenye Kijiji cha Tulieni Kata ya Jamhuri Lindi mjini.
 Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Kata ya Jamhuri Lindi mjini, wakimsikiliza Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Mke wa Rais, Mama Salma Kikwete (hayupo pichani), alipozungumza nao katika kikao cha ndani, kwenye Ofisi ya CCM, tawi la Tulieni katika Kata hiyo leo, Feb 19, 2013.
 Bi, Fatuma Jaluo (78) akifuatilia kwa makini msafara wa Mke wa Rais Mama Salma Kikwete ulipopita karibu na nyumbani kwake, katika kijiji cha Tulieni, Kata ya Jamhuri wilaya ya Lindi mjini leo, Feb 19, 2013.
 Kina Mama wa CCM, wakishiriki kula kiapo cha mwanachama wa CCM wakati wanachama wapya waliokabishiwa kadi na Mama Salma Kikwete walipokuwa wakipa, kwenye mkutano uliofanyika kijiji cha Tulieni,  kata ya Jamhuri wilaya ya Lindi mjini, leo Feb 19, 2013. Kutoka Kushoto ni Fatuma Mohamed, Aswila Ditopile na Zitta Maliyaga ambaye ni Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Lindi.

 Vijana 36 waliokuwa wanachama wa CUF na kuamua kuhamia CCM, wakimsiliza mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipohutubia mkutano wa hadhara jana, Feb 19, 2013, kwenye Kijiji cha Mitandi, Kata ya Mbanja, Lindi mjini.
Baadhi ya waandishi wa habari, waliopo kwenye ziara ya Mama Salma Kikwete mkoani Lindi, wakiwa wameketi kwenye mkeka wakati wa mkutano uliofanyika kijiji cha Tulieni, Kata ya Jamhuri Lindi mjini leo Feb 19, 2013. Kushoto ni Mwenyeji wa kijiji hicho, Khalfan Dimoso. (Picha zote na Bashir Nkoromo).

No comments:

Post a Comment