May 6, 2013

NG'OMBE HAZEEKI MAINI,,,"Nimezama mapenzini na ninamuoa Gina," aliongeza. "Nina miaka 86 lakini nina moyo wa mwanaume kijana."
Di Stefano alifiwa na mkewe miaka nane iliyopita. Alisema wanae hawataki aoe, lakini yeye hajali kuhusu hisia zao. "Ninachoangalia sasa ni maisha yangu na sio kitu kingine chochote.
Akiwa kama mchezaji, Di Stefano alishinda makombe matano ya ulaya na Real Madrid kutoka mwaka 1956 na 1960. Akiwa kama kocha, aliiongoza Boca Juniors na Valencia kushinda makombe ya ligi.
Raisi wa heshima wa Real Madrid Alfredo Di Stefano, ambaye atatimiza miaka 87 mwezi Julai, anatarajiwa kumuona mwanamke mwenye miaka 36 ambaye alimsadia kutaarisha kitabu cha maisha kilichotolewa mwaka 2010. Di Stefano, ambaye amekuwa akipambana na matatizo kadhaa ya afya, amesema ucheshi wake ndio uliomvutia mwanamke huyo kuwa mpenzi wake. Akitajwa kama mmoja wa wachezaji bora wa muda wote, mzaliwa wa Argentina Di Stefano alisema alikuwa anajiandaa kumuoa Gina Gonzalez mwenye miaka 36 wiki chache zijazo "kwa dababu nahitaji kuwa na mwenza na pia nimekuwa mpweke kwa miaka 8 sasa", alinukuliwa na gazeti la El Mundo.

No comments:

Post a Comment