katika mahojiano aliyoyafanya na kituo kimoja cha redio Bongo, Aggy, amefunguka kuwa akiwa safarini nje ya Bongo alipewa taaraifa za kupotea kwa Digital Camera ambayo anadai ndiyo ilitumika kurekodia video hiyo na baada ya uchunguzi kufanywa na watu wake wa karibu iligundulika kuwa mwigizaji huyo ndiye anahusika na kupotea kwa kamera hiyo huku pia akidai ndiye aliyefanya kazi ya kusambaza video hiyo kwenye vyombo vya habari na mitandao kadhaa.
"Nilipewa taaraifa ya kupotea kwa kamera hiyo, nina hakika atakuwa sintah ndiye aliyefanya kazi ya kuisambaza, awali nilitaka kuchukua hatua juu ya jambo hilo lakini nikashauriwa na watu wangu kuwa nisifanye hivyo, kwa kweli najisikia vibaya lakini namwachia Mungu". alisema.
No comments:
Post a Comment