Jul 27, 2012

IJUMAA SEXIEST GIRL COMPETITION.....

WEMA SEPETU....
AUNT EZEKIEL....
JACK WOLPER....
AGNES GERALD....
WASHIRIKI watatu ambao ni kati ya wanne waliobaki kwenye Shindano la The Ijumaa Sexiest Girl, Aunt Ezekiel, Agnes Gerald na Jack Wolper juzi walitembelea moja ya maduka ya vidodozi ya Shear Illusions lililopo Mlimani City jijini Dar. Wakiwa dukani hapo, mastaa hao walipewa ofa ya kununua vipodozi mbalimbali kwa bei poa huku wakisifia mali bora zinazopatikana hapo. Aidha, mastaa hao waliwapongeza Shear Illusions kwa kuwa kampuni inayouza vipodozi safi visivyo na madhara kwa wanawake tena kwa bei nafuu. Wakati huohuo, mratibu wa shindano hili, Imelda Mtema amesema wiki hii hakuna mshiriki anayetoka hivyo wadau waendelee kupiga kura ili wiki ijayo ipatikane Tatu Bora. Unachotakiwa kufanya ni kumpigia kura mrembo anayestahili kutoka kwa kuandika jina lake kisha kulituma kwenda namba 0786 799120. Kumbuka shindano hili limedhaminiwa na Kampuni ya Shear Illusions na Ukumbi wa Burudani wa Dar Live uliopo Mbagala, Dar.

No comments:

Post a Comment