Aug 1, 2012

KAPTENI KOMBA AREJEA NCHINI.


MBUNGE wa Jimbo la Mbinga Magharibi Kepteni John Komba hatimaye amerejea nchini baada ya kufanyiwa upasuaji nchini India.
Mwandishi mwandamizi wa habari za burudani Jimmy Chika alimtembelea nyumbani kwake Mbezi beach hivi karibuni na kufanya naye mahojiano ambapo alimweleza alifanyiwa upasuaji wa nyonga baada ya kupata ugonjwa uliosababisha mifupa kusagana sehemu ya nyonga.
Komba ambaye pia ni Mkurugenzi wa kundi la sanaa la TOT alisema upasuaji wa uliochukua takriban masaa matano ulifanyika katika Hospitali Apollo nchini India.
Hata hivyo alikanusha taarifa zilizowahi kuandikwa na magazeti ya Bongo kwa alizidiwa sana na ugonjwa wa figo na kulazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi ICU nchini humo.

No comments:

Post a Comment