Sep 3, 2012

JACK WA MAISHA PLUS NAE HOI KITANDANI,,,

MSHIRIKI wa Shindano la Maisha Plus Season II, Jacqueline Dastan ‘Jack wa Maisha Plus’ ni mgonjwagonjwa.
Habari zinasema nyota huyo anasumbuliwa na malaria pamoja na homa ya matumbo ‘typhoid’.
Jack alinaswa na kamera yetu hivi karibuni nyumbani kwake, Kijitonyama, Dar ambapo alikuwa hoi kitandani na akaeleza kuwa anasumbuliwa na magonjwa hayo kwa muda sasa.
Aidha, Jack alisema alipata matibabu kwa saa kadhaa katika Zahanati ya Micco iliyopo Kinondoni ambapo aliruhusiwa na kurudi nyumbani, mpaka sasa anaendelea na dozi ya vidonge.
“Yaani namshukuru Mungu sana, kwa sasa naendelea vizuri kwani jana hali yangu haikuwa nzuri, naona dozi niliyoianza inanipa nafuu,” alisema Jack.
Kwa upande mwingine, Jack alisema sababu kubwa ya kukumbana na magonjwa hayo ni kutokana na kubadili hali ya hewa kwani hivi karibuni alikwenda nyumbani kwao, Morogoro ambako alikaa kwa siku kadhaa na baridi ilikuwa kali tofauti na Dar.
“Hivi karibuni nilikwenda nyumbani Morogoro kula Sikukuu ya Idi. Kwa sasa hali ya Moro ni ya baridi sana hivyo baada ya kurudi tu hapa ndiyo nikaanza kusikia maumivu ya tumbo na kichwa,” alisema Jack.

No comments:

Post a Comment